SALA YA KUOMBA NEEMA KWA NJIA YA

MAOMBEZI YA MTUMISHI WA MUNGU

PAPA YOHANI PAULO WA PILI

Ee Utatu Mtakatifu,
tunakushukuru kwa kuwa umelipatia Kanisa
Papa Yohani Paulo wa Pili,
na kwa kuwa umefanya ving’ae ndani yake
mapendo na huruma yako ya kibaba,
utukufu wa Msalaba wa Kristo,
na mng’ao wa Roho wa Upendo.
Yeye, akijiaminisha kabisa katika huruma yako kuu isiyo na mipaka,
na katika maombezi ya kimama ya Mama Bikira Maria,
ametuonyesha sura hai ya Kristo Mchungaji Mwema,
na ametuonyesha utakatifu
kama upeo wa juu kabisa wa maisha ya kawaida ya kikristu,
na kama njia ya pekee ya kuweza kufikia muungano kamili wa milele pamoja nawe.
Tunakuomba utupatie, kwa maombezi yake na kufuatana na mapenzi yako,
neema ambazo tunakuomba,
tukiwa tumejawa na tumaini kubwa kwamba mapema atakwezwa
na kuweza kuhesabika kati ya watakatifu wako.
Amina.
 

Imethibitishwa kwa mamlaka ya Kanisa
Camillo Kardinali Ruini,
Askofu mkuu mwandamizi wa Baba Mtakatifu
Kwa dayosisi ya Roma

 
• Sala – kiswahili

© Libreria Editrice Vaticana

Preghiera