Ee Utatu Mtakatifu,
tunakushukuru kwa kuwa umelipatia Kanisa
Papa Yohani Paulo wa Pili,
na kwa kuwa umefanya ving’ae ndani yake
mapendo na huruma yako ya kibaba,
utukufu wa Msalaba wa Kristo,
na mng’ao wa Roho wa Upendo.
Yeye, akijiaminisha kabisa katika huruma
yako kuu isiyo na mipaka,
na katika maombezi ya kimama ya Mama Bikira
Maria,
ametuonyesha sura hai ya Kristo Mchungaji
Mwema,
na ametuonyesha utakatifu
kama upeo wa juu kabisa wa maisha ya kawaida
ya kikristu,
na kama njia ya pekee ya kuweza kufikia
muungano kamili wa milele pamoja nawe.
Tunakuomba utupatie, kwa maombezi yake na
kufuatana na mapenzi yako,
neema ambazo tunakuomba,
tukiwa tumejawa na tumaini kubwa kwamba
mapema atakwezwa
na kuweza kuhesabika kati ya watakatifu wako.
Amina.
Imethibitishwa kwa mamlaka ya Kanisa
Camillo Kardinali Ruini,
Askofu mkuu mwandamizi wa Baba Mtakatifu
Kwa dayosisi ya Roma
• Sala – kiswahili
© Libreria Editrice Vaticana
indietro
|